Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Richard Rwehumbiza amesema Halmashauri kupitia Baraza la Madiwani imetenga Milioni 240 kwa ajili ya kukamilisha Vituo vya Afya ambavyo moja wapo ni kituo cha Afya cha Irisya ambacho ujenzi wake upo hatua za mwisho za ukamilishaji na kimeanza kutumika baadhi ya Vyumba kutokana na uhitaji mkubwa wa Kituo hicho cha Afya Hayo yamesemwa katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Peter Serukamba wakati wa ziara yake katika vijiji vya Irisya kukagua kituo cha Afya,Munyu kuzungumza na wananchi,Kutembelea Shule ya msingi shikizi Senga Senga,kutembelea ujenzi wa Madarasa Msungua na baadae kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao kijiji cha Kipunda ambapo kero yao kubwa ilikua ni Barabara na kumalizia ukaguzi wa ujenzi Madarasa Shule ya Msingi Kintandaa yanayogharimu Milioni 3.1 na iko hatua ya Upauaji.Aidha Mkuu wa Mkoa amepongeza wananchi kwa kujitolea katika maeneo mengi kuanzisha miradi mbalimbali ya Maendeleo kadri nguvu zao zitakapoishia na kuiomba Serikali kupitia Halmashauri kumaliza majengo hayo huku akimuomba Kaimu Mkurugenzi kupokea mahitaji yao ili miradi iweze kukamilishwa kupitia mapato ya ndani.Kwa upande wake Emanuel Kikoti Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Ikungi akisoma taarifa ya Ujenzi wa mradi wa Kituo cha Afya Irisya amesema ujenzi wake umegharimu Takribani Milioni 500."Kituo cha afya tayari kimeanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje, huduma za chanjo na huduma za kulaza IPD, Pia tunategemea kuanza kutoa huduma za uzazi na Mpango ni kuongeza kwa kadri majengo yatakavyokuwa yanakamilika."Amesema Kikoti.MWISHOImetolewa na;Afisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi28/11/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa