Mkurugenzi msaidizi wa Tiba TAMISEMI Dkt. Chawote akiambatana na timu inayosimamia shughuli za afya ameagiza kukamilishwa kwa miradi mbalimbali ya hospitali, vituo vya afya, zahanati pamoja na kuhakikisha uwepo wa vifaa tiba ili kupunguza na hatimaye kumaliza tatizo la wananchi kukosa tiba katika baadhi ya maeneo.Hayo yamesemwa leo tarehe 04 Aprili, 2024 katika ziara ya usimamizi shirikishi huduma za afya na miradi inayotekelezwa mwaka wa fedha 2023/2024 katika Wilaya ya Ikungi.Timu hiyo imekagua nyaraka mbalimbali za hospitali ya wilaya ya Ikungi,vituo vya afya pamoja na zahanati na baadae kutembekea mradi wa ujenzi wa Zahanati uliopo hatua ya ukamilishaji na unaotarajiwa kugharimu milioni 50 kijiji cha Ighuka na Mradi wa ujenzi wa Zahanati Kijiji cha Nkuninkana unaogharimu milioni 50 na upo hatua za ukamilishaji.Mkurugenzi amepongeza juhudi na hatua za ujenzi wa Hospitali, vituo vya afya pamoja na zahanati hizo kutokana na usimamizi mzuri unaofanyika na kuwaomba kuongeza Kasi ya ukamilishaji wa majengo hayo na kuanza kutumika kwa wakati."Serikali inapotoa fedha Kwa ajili ya ujenzi wa miradi hii tunachotegemea ni kuona majengo hayo yanafanya kazi na sio vinginevyo kwani fedha zinakuja Kwa awamu na kwa bajeti" amezungumza Mkurugenzi Mwisho Mganga Mkuu Wilaya ya Ikungi Dkt Doricilla amepongeza timu hiyo kufika katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na kukagua miradi hiyo na kuahidi kuchukua yote ambayo yanapaswa kutekelezwa na kuyafanyia kazi mapema zaidi ili kuhakikisha vituo vyote na zahanati zinafanya kazi Kwa viwango vinavyostahili na kuomba serikali kuongeza watoa huduma za afya katika Wilaya ya Ikungi kutokana na upungufu uliopo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma Kwa wakati.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa