Afisa elimu ndg Margareth Kapolesya na Afisa mipango ndg Faraja Maliga wametembelea miradi ya BOOST Ifyamahumbi kata ya Mtunduru na Ituru kata ya Mtavira hapo jana 21juni 2023.
Katika ziara hiyo maafisa hao wamesisitiza mafundi waongeze spidi ya umaliziaji wa maboma hayo kwa haraka na kuwakabidhi funguo ifikapo tarehe 25 Juni 2023.
Pia Afisa mipango ameongeza kwa kusema kama nguvu ni ndogo ,waongeze mafundi wengine ili kazi uendelee na kukabidhi funguo kwa wakati.
Mwisho mafundi hao wamesema kuwa wao wanasubiri mabati tu yafike waanze kupaua na kumalizia sehemu zilizobaki.pia wamesema kuwa mpaka walipofikia hawana changamoto yoyote.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa