Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi Afungua mafunzo ya mradi wa pamoja wa kuongeza kasi ya uwezeshaji wa wanawake wa kijijini kiuchumi Wilayani Ikungi yanayotolewa na Kampuni ya KIVULINI.Akizungumza na Wanamabadiliko kutoka katika kata tano lengwa na Mradi huo wakati anafungua mafunzo Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi Tarehe 24 Agosti,2023 Mkurugenzi amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa wanamabadikiko kwani yatasaidia mradi huo kufanyika kwa ufanisi na juhudi kubwa lengo kuu ikiwa ni pamoja na kubadili fikra za jamii nzima kuwa na mtazamo chaya.Bi-Haika Massawe ni Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi amezungumza na waandishi wa Habari na kusema kuwa mafunzo yatachukua siku tano na yanalengo la kumjenga mwanamke wa Ikungi katika maswala ya Uongozi,usawa wa kijinsia,Elimu ya ukatili,Lishe kwa familia na mengineyo yanayohusu jamii kwa Ujumla.Afisa maendeleo ameongeza na kusema lengo lingine pia ni kutokomeza mimba za utotoni ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto na Kuchukua Hatua kwa kutumia mamlaka au nguvu za kisheria.Lakini pia aliwasisitiza viongizi wa kijamii,wa Dini Wataalamu wa fani mbalimbali,Wanamabadiliko,Jamii kwa Ujumla kuripoti mapema matukio ya ukatili katika jamii zao ili kuwezesha mamlaka kuchukua hatua kwa wakati.Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya WFP,IFAD,FAO na UN Women kwa ufadhili wa serikali ya Norway na Sweeden na Kauli mbiu ya ya mafunzo haya ni "Kila mtu ana sauti je unatumiaje sauti yako?"Mwisho Mkurugenzi aliishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushirikiana vyema na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kupandisha uchumi nchini kote.MWISHOAfisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya IkungiTarehe 24/08/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa