Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi awataka watumishi wa serikali katika kata mbalimbali wilaya ya Ikungi kuzingatia maadili na nidhamu.Akizungumza na watumishi (Watendaji wa vijiji na kata,Walimu wa msingi na sekondari) kata ya Kituntu katika kikao cha ndani leo tarehe 07 March 2023 amewataka watumishi kuzingatia maadili ya utumishi pamoja na maadili ya wanafunzi katika kata hiyo na kata zingine kwa ujumla lengo ikiwa ni kuepukana na madhara mbalimbali ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na utovu wa nidhamu"nitasisitiza hilo na sitoishia kata hii pekee kata zote nitafika maana msingi mzuri wa maendeleo ni nidhamu kwanza hata kukamilika kwa miradi mbalimbali inayotolewa kwa juhudi za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan."alisema Kijazi.Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo pia alipata wasaa wakufanya mkutano na wananchi wa Kata ya Utaho ambapo ameahidi kukukamilisha mfumo wa maji ulioanzishwa na kufadhiliwa na shirika la Uturuki na Quet,kwa upande wa zahanati ameahidi kuongeza Milioni 1 kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa zahanati na kuleta watumishi na vifaa vya kutolea huduma "fedha zijazo Halmashauri ya wilaya itatenga million 500 kwa ajili ya kupanua ujenzi wa zahanati ya utaho...Mkurugenzi pia amewataka wazazi kuchangia chakula kwa wanafunzi ikiwa ni agizo la mkuu wa Mkoa ili kutengeneza lishe (afya) ya mtoto na kuepusha kwenda na kurudi nyumbani kwani wengine wanakaa mbali na shule...Kabla ya mkutano huo Mkurugenzi Kijazi akiongozana na Mhe Diwani Kalebu na viongozi wa kata na Kijiji ametembelea shule ya msingi Samamba ,Shule ya Msingi Utaho na zahanati ya Utaho kuangalia hali ya ujenzi unaoendelea na kuangalia mfumo wa maji uliojengwa na wafadhili ili kuhakikisha wananchi wa utaho wanapata maji kwa wakati.
MWISHO
fisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi
07/03/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa