Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi amewataka watumishui wa halmashauri hiyo kuwa na ushirikiano na kuongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato katika Wilaya hii.
Akizungumza mara baada ya watumishi hao kusoma taarifa za kila idara mbele ya mkurugenzi leo tarehe 05,Desemba,2022 Kijazi amesema kuwa usirikiano unasaidia kukuza mshikamano na mahusiano baina ya viongozi na mashirika mbalimbali pamoja na wadau katika kuleta maendeleo ya wilaya ya Ikungi na Mkoa wa Singidsa Kwa ujumla.
Aidha kwa upande wao wakuu wa idara wameahidi kushirikiana kikamilifu kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaongezeka na hatimaaye kuleta maendeleo katika Wilaya ya Ikungi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa