Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri,Afisa Kilimo Wakiwa na Mkuu wa Masoko na mauzo ( Head of Sales and Marketing) wa Kampuni ya Minjingu wajadiliana juu ya upatikanaji na matumizi ya mbolea ya Minjiku katika Msimu wa kilimo 2023/2024. Wakijadiliana katika ofisi ya Mkurugenzi Leo tarehe 08 Juni 2023 Kijazi ameishukuru kampuni hiyo kwa kuonesha nia ya kuanza kusambaza Mbolea hiyo kwa mfumo wa Ruzuku ya serikali kwa wakati husiki. Aliendelea kusema kuwa katika msimu uliopita wa 2022/23 wakulima waliowengi walipata changamogo sana ya kupata mbolea za aina zote hasa ya kupandia na kukuzia. Hivyo ameahidi kumpa Afisa masoko na Mauzo wa kampuni hiyo ushirikiano ili wakulima kupata huduma kwa wakati.Pia Afisa Kilimo Wilaya Ndugu Gurisha Msemo aliweza kusema kuwa wao kwa sasa wameanza kuhamasisha wakulima kujiandikisha katika Daftari la ruzuku ya Mbolea na pia kuhakiki taarifa za wakulima kwa msimu wa mwaka jana kwenda msimu wa kilimo wa 2023/24.Gurisha Alitoa takwimu kuwa hadi sasa ni wakulima 11,123 ndio ambao wamejiandikisha lakini zoezi bado linaendelea ili wakulima wote kupata huduma kwa wakati.Aidha amesema wameanza kubaini wakala wa pembejeo na vyama vya ushirika vitakavyoweza kutoa huduma hiyo ya kuuza mbolea kwa njia ya Ruzuku kwa kusogeza huduma hiyo karibu na wakulima.Afisa wa Masoko wa kampuni hiyo ametoa ahadi ya kushirikiana kwa karibu sana na Halmashauri ya Ikungi ili kupata mbolea kwa wakati katika msimu wa 2023/24.Hivyo ameomba aendelee kupewa ushirikiano ili mkulima aweze kupata huduma kwa karibu na wakati.Aliendelea kusema kuwa mbolea ya Kampuni ya Minjingu ni mbolea organic hivyo ni nzuri sana kwa ardhi yetu na mazao tunayozalisha.MWISHO Afisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi08/06/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa