Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi amemkabidhi PikiPiki 3 Aina ya Boxer Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Dkt Solomon Michael...
Makabidhiano hayo yamefanyika Tarehe 5 Octoba 2022 katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya hiyo huku akimwomba Mganga Mkuu kuwa PikiPiki hizo zitumike katika kufatilia huduma za Afya pamoja na lishe katika wilaya hiyo..
Kijazi ameongeza na kusema kuwa PikiPiki hizo zimetolewa na serikali kwa ajili ya shughuli maalumu za kiafya na zitumike kadri watakavyopewa maagizo na Mganga huyo...
Kwa upande wake mganga mkuu amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa kuthamini Idara ya Afya kutokana na umuhimu wake katika kuifikia jamii kiurahisi kwa kutumia usafiri huo na kupunguza changamoto za kiafya kama sio kuzimaliza kabisa.alisema Mganga Mkuu...
Solomoni aliongeza na kusema kuwa Moja ya PikiPiki walizopewa itatumika katika kufatilia shughuli zote za ujenzi wa vituo vya afya na miundo Mbinu yote inayohusiana moja kwa Moja na maswala ya kiafya katika halmashauri hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa