Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ngd Justice L.Kijazi afungua mafunzo ya mfumo mpya wa manunuzi NEST unaorahisisha shughuli za manunuzi mbalimbali.Mfumo wa NEST ni mfumo mpya wa manunuzi ambao umeanza kutumika rasmi Tarehe 01 October 2023 ambapo wakuu wa idara na vitengo pamoja na watumishi wengine wanapaswa kuufahamu mfumo na kufanya shughuli zote za manunuzi kupitia mfumo huo mpya.Akizungumza na Wakuu wa Idara pamoja na baadhi ya watumishi hii leo Tarehe 05 October 2023 katika ukumbi wa mafunzo Halmashauri amesema kuwa kila mtumishi azingatie mafunzo hayo kwani manunuzi hayatofanyika kwa njia nyingine yeyote zaidi ya mfumo wa NEST.Kwa upande wake Afisa Manunuzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Mariam Haroun ameongeza na kusema kuwa serikali imeleta mfumo huu kuepusha maswala ya Rushwa,Wizi,na kuongeza uharaka tofauti na zamani ambapo manunuzi yalikuwa yanachukua mlolongo mrefu zaidi.Mafunzo hayo yamefanyika chini ya Usimamizi wa Idara ya Manunuzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakishirikiana na TEHAMA ambapo utekelezaji wake unaanza mara moja mara baada ya mafunzo hayo kufanyika.MWISHO Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi05/10/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa