Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi pamoja na wakuu wa idara watembelea katika kata ya Mgungira kuzungumza na watumishi na kuona shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile zahanati ya Mgungura, ghala la mbegu na mbolea (Ikungi) na baadae kutembekea mashamba ya wakulima wa Mpunga ambayo yamevamiwa na ndege aina ya kwelea kwelea.Ziara hiyo imefanyika tarehe 12 Aprili, 2024 katika kata ya Mgungira ambapo Mkurugenzi mtendaji amewaelekeza wakulima kulima kwa kufuata kanuni bora za kilimo lakini pia kuendelea kufukuza ndege waharibifu wakati wakisubiri ndege ya serikali itakuja wiki ijayo kwaajili ya kuangamiza ndege hao waharibifu wa mazao.Sambamba na hilo amewaomba wakulima kutokuuza mazao yao kiholela yakiwa bado yapo shambani badala yake wasubiri yakomae, wavune na kusubiri bei nzuri ili kupata tija katika mazao yao.Kwa upande wake Afisa Kilimo Ndg. Gurisha Msemo akizungumza na mwandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo amesema kuwa kuna haja ya wakulima kutumia mbegu bora za rusuku pamoja na mbolea inayotolewa kwa bei nafuu serikalini ili kuhakikisha tunakuza uchumi wetu mkoa wa Singida hususani Wilaya yetu ya Ikungi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa