Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi amewasisitiza watumishi kujua na kufuata sheria za kazi zilizowekwa wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku kwa kuhakikisha wanafika maofisini kwa wakati na pia kuwa na mahudhurio mazuri kazini.Ziara ya Mkurugenzi ya kusikiliza na kutatua kero za watumishi na wananchi leo tar 13 Mei, 2024 imeanzia katika shule ya msingi Kipunda kwa kufanya mkutano wa ndani na watumishi ambapo kero zilizowasilishwa na watumishi waliohudhuria mkutano huo ambapo Mkurugenzi mtendaji amesema kuwa kufuata sheria za kazi kutatuweka salama wakati wote.Mkurugenzi amewahakikishia watumishi kuwa changamoto ya uhaba wa watumishi ataendelea kushugulikia kwa kuwaleta watumishi anaopewa kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa kama ilivyo kwenye kata ya Mtunduru, hivyo wawe na subira.Hata hivyo wamewasilisha changamoto ya uhaba wa vitendeakazi kama vile viti, meza na mabenchi kwenye Zahanati ya Kipunda, vitu hivyo vitaletwa kwenye Zahanati, Changamoto ya uhaba na uchakavu wa miundombinu mashuleni, kwenye majosho pamoja na uchache wa nyumba za watumishi, matundu ya vyoo na baadhi ya miradi kukwamia kwenye hatua ya umaliziaji atabishughulikia kwa wakati"Miradi iliyotekelezwa kwenye kata ya Mtunduru ni ya dhamani ya Bilioni 1.3 miradi hii ni ujenzi wa zahanati na madarasa, kwa fedha za wafadhili zimetumika milioni 500 na milioni 120 madarasa nane shule ya Sekondali mtunduru hivyo serikali inajitahidi sana kufikia adhima ya kumuinua mtanzania" amezungumza KijaziAfisa Maendeleo ya jamii Wilaya Bi. Haika Massawe kwa upande wake amewasisitiza watumishi hususani walimu juu ya kuzingatia suala la uadilifu kwao wenyewe na kwa watoto wanaowafundisha, sambamba na hilo alizitaka shule na vituo vya kutolea huduma za afya vyenye miradi kuzingatia matumizi ya fedha za miradi husika na kuhakikisha kuwa inakamilika kwa wakati. Aidha katika mkutano na wananchi Mkurugenzi alianza kwa kuwajuza wananchi juu ya kazi nzuri ambayo Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameifanya katika Wilaya ya Ikungi ikiwemo kupandisha bajeti ya Halmashauri kutoka billion 28 mpaka kufikia Billion 41 na pia kutoa zaidi ya Bilioni 1 kufanikisha miradi mbalimbal
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa