Halmashauri ya wilaya ya ikungi hapo jana 14 februari 2023,waheshimiwa madiwani wamepitia na kujadili rasimu ya bajeti ya ujenzi wa barabara na makadilio ya mapato na matumizi ya fedha za sekta ya maji katika wilaya hiyo.
Meneja wa TARURA Inj Ally R. Mimbi amesema kuwa Tarura imejipanga kutengeneza barabara na madaraja kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwabajeti ya sh 4,472,547,262.47.
Katika kusema hayo Maneja wa TARURA ameomba kuidhinishiwa bajeti hiyo ya Tsh 4,472,547,262.47kwa ajili ya matengenezo ya barabara miradi ya maendeleo ,ujenzi wa madaraja ,fedha za usimamizi wa miradi na fedha za kuendesha shughuli za ofisi.
Aliongeza kuwa barabara hizo ambanzo ziko katika bajeti hiyo ni Mungaa-ntuntu-Mang'onyi,Issuna-Ngongosoro-Ilolo,Mtamaa-Minyuge-Mtavira na Mandimu-mnane.Pia amesema barabara zingine zitakazo kuwa kwenye matengenezo ni Ikungi mjini,Ujaire-lighwa,Mkiwa-choda ,Misughaa-Msule Sambaru ,Kipunda -Bunku,Mtunduru _Minyuge,Ikhamo -Mayaha-Ighombwe ,Sepuka-italala,Puma-Iglansoni,Balimaloage,Iglanson-Mkenene -Iyumbu pamoja na barabara ya Mnang'ana -mwasutianga.
Pia meneja wa RUWASA Inj hopeness E.Liundi amesema kuwa bajeti yao ya mwaka wa fedha 2023/2024 ni tsh 2,312,872,728.61. kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo ukamilishaji wa miradi ya maji vijijini inayoendelea na ujenzi wa miradi mipya iliyopangwa kutekelezwa katka wilaya .
Waheshimiwa Madiwani wameridhia na bajeti hiyo na kuipitisha bila mapungufu yoyote ili ikawakilishwe eneo husika.
Pichani ni Inj Ally R.Mimbi kushoto,Inj Hopeness e.liundi kulia na chini ni waheshmiwa Madiwani kushoto na wakuu wa idara kulia.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa