Watendaji wa Kata, Vijiji na Mafisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wamuahidi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Peter Serukamba kuongea zaidi ya Hekari 2200 za kilimo katika kata zao msimu huu wa kilimo 2023/2024.Hayo yamesemwa na Kila Mtendaji wa kata mbele ya Mkuu wa Mkoa katika kikao kazi mapema leo hii Tarehe 04 Desemba 2023 Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi alipokua akizungumza na watumishi wa Wilaya hii.Serukamba amesema kuwa Moja ya adhima kubwa ya Mkoa wa Singida ni kuwa na zao kuu linalotegemewa na kututambulisha katika kila Mkoa ili kukuza uchumi wetu."Hivyo nilazima kuwahamasisha wananchi hususani vijana wajikite kwenye kilimo cha mazao ya biashara na chakula ili kuongeza uzalishaji hasa zao la Alizeti kutoka asilimia 50, msimu uliopita hadi kufikia 70, msimu huu (2023/24)"Amesema Serukamba.Afisa Kilimo Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha Msemo ameeleza kwamba watajitahidi kufikisha mbegu kila kata wakulima walipo mbegu mpya aina ya Haysan, itakayouzwa kwa bei ya ruzuku kwa ajili ya kutoa nafuu kwa mkulima kuweza kuzalisha kwa wingi zao la Alizeti.Pia Afisa Kilimo amesisitiza umuhimu wa matumizi ya mbolea kwa ajili ya kuleta tija na kuongeza uzalishaji wa mbegu za Alizeti shambani ili kukuza sekta ya kilimo Wilayani Ikungi.MWISHO IMETOLEWA NA;AFISA HABARI (W)IKUNGI04/12/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa