Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Singida na Wilaya ya Ikungi watoa onyo Kali Kwa wafugaji wanaowanyanyasa wawekezaji wa eneo la kilimo Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.Hayo yamesemwa baada ya kuwepo kwa tuhuma kutoka Kwa muwekezaji akilalamika kuharibiwa Kwa mazao yake mara baada ya kupanda Ulezi, Korosho na Mahindi katika eneo alilokabidhiwa kisheria Kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Kijiji Cha Ulyampiti Pamoja na Wilaya ya Ikungi Kwa ajili ya kilimo.Wafugaji hao kutoka Kijiji Cha jirani Cha Mwau wanadai wanachunga katika eneo hilo kwani hawamtambui muwekezaji na eneo hilo ni lakwao hivyo hawaoni kosa laoKatika ziara yake ya kikazi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Peter Joseph Serukamba amepata wasaa wa kuwasikiliza pande zote viongozi wao pamoja na wananchi na kubaini Kuwa mipaka inayotenganisha Vijiji hivyo viwili vimepimwa na wananchi wanapaswa waonyeshwe mipaka hiyo."Naagiza Afisa Ardhi kutoka Mkoani akishirikiana na wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kufika mapema katika mpaka huo kuwaonyesha wananchi mipaka yao ili kuondokana na Mgogo huu unaovunja moyo wawekezaji wa maeneo hayo."Amesema Mkuu wa Mkoa
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa