Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson akishirikiana na Mkururugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi wameahidi kutatua changamoto ya maji inayowakabili Kijiji cha Issuna A ndani ya Wiki mbili wakishirikiana na RUWASA.Hayo yamesemwa katika ziara ya Mkuu wa Mkoa tarehe 19 alipokuwa akitembelea vijiji vitatu Choda,Issuna A na Issuna B kuhamasisha wananchi kuruhusu fursa za uwekezaji katika vijiji vyao Ili kukuza maendeo kwa haraka.Mkuu wa Wilaya amesema watafanya ziara za mara kwa mara kusikiliza na kutatua changamoto zao kadri watakavyopata muda lengo ikiwa ni kukuza maendeleo wilayani Ikungi.Aidha Mkuu wa Mkoa amesema Ikungi imepata Wawekezaji wapya ambao ni wawekezaji wanaohitaji kuwekeza kwenye kilimo kwenye zaidi ya Ekari 10,000 ambapo amehamasisha wananchi kuchukua hiyo kama fursa kwani wawekezaji wameomba ekari 10700 Issuna A,Issuna B 1500 pamoja na 7000 Kutoka katika Kijiji cha Choda na waekezaji hao ni wapya na baadhi wenyeji lengo ikiwa ni kukuza sekta ya Kilimo Wilaya ya Ikungi.Afisa kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha Msemo amezungumza na Afisa Habari na kisema moja ya faida za uwekezaji huo wa kilimo wilayani Ikungi ni pamoja na Kujifunza teknolojia mpya za kilimo cha kisasa,namna ya matumizi ya mbegu Bora,na pia ni ajira kwa wakazi wa Ikungi,Singida na Nchini kwa ujumla.Bwana Ambrose Ngonyani ni Afisa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi amesema kuwa taratibu zote za upimaji zitafuatwa bila kuvunja Sheria za uthamini wa ardhi na watakaohusika kulipwa fidia watalipwa kwa wakati.Ziara hiyo iliambatana na viongozi mbali mbali wa mkoa na Wilayani ikiwa ni pamoja na Viongozi wa chama cha mapinduzi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama.Afisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi19/07/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa