Baadhi ya wanamchi wa kijiji cha Issuna Wilaya ya Ikungi walamika kuwepo kwa wawekezaji katika kijiji chao na kijiji jirani hali inayopelekea kuondolewa mashamba yao bila utaratibu na wengine kudai tayari kesi zao ziko mahakamaniHayo yameibuka katika mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Thomas Apson alipokuwa akisikiliza kero za wananchi katika kijiji hicho tarehe 09 Aprili, 2024 ambapo baadhi ya wananchi wamesema kuwa kumeibuka utaratibu wa watu kuuza mashamba ambao unapelekea migogoro ya ardhi kati ya wananchi na wawekezaji ambao wanazunguka eneo la kijiji cha choda Issuna A na Issuna B Hali hiyo imepelekea wananchi kuhoji mashwali mengi kwa Afisa ardhi wa Wilaya kutaka kujua taratibu gani zinatumika wawekezaji kupewa mashamba bila idhini ya wananchi na wengine wakilalamika kutokupewa taarifa juu ya uwepo wa wawekezaji hao.Afisa ardhi wa Wilaya ya Ikungi Bwana Salum amejibu na kusema kuwa Moja ya vipaumbele vya Mhe.Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuruhusu wawekezaji nchini ili waweze kushirikiana na wazawa kukuza maendeleo nchini, na Mkoa wa Singida ni Mkoa wa kimkakati kwenye swala la kilimo cha alizeti ili kutatua uhaba wa mafuta na Wilaya kushirikia na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba kipindi hicho walipita na kuhamashisha jamii juu ya umuhimu wa uwekezaji katika vijiji hivi."Hivyo jukumu letu ni kutafta wawekezaji ambao wanakidhi vigezo kwa kushirikiana na serikali ya kijiji husika na kutenga maendeneo yanayofaa kwa ajili ya kuwekeza mazao mbalimbali hasa kilimo cha alizeti na kulipa fidia kwa wananchi wenye maeneo husika" amezungumza Afisa ArdhiKwa upande wake Afisa Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi.Edina Aivan Palla ameongeza na kusema kuwa panapotokea mikutano ya kijiji, ujio wa viongozi pamoja na mikutano mingine yote wananchi wanajitokeza kwa wingi kwani ndiko taarifa mbalimbali hutolewa.Mwisho Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson Amewataka wanachi kutambua na kuthamini mchango wa Mhe. Rais wa Tanzania kwani amekuwa akifanya mengi mazuri nyakati zote hadi hivi sasa katika mwaka wake watatu kwenye uongozi wake na pale wanapotazama mapungufu watazame na mazuri yaliyofanyika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa