Wananchi wa kata ya Iglansoni wilayani Ikungi waomba kutatuliwa kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa wakati ili kuwezesha kukua kwa maendeleo katika kata yao.Baadhi ya changamoto hizo ambazo wananchi wamameeleza kuwa zimekua kero kwao ni pamoja na upatikanaji wa mbolea kwa wakati, kubadilika kwa utaratibu wa utoaji vyeti vya kuzaliwa, ukosefu wa umeme vijijini, ukosefu wa shule shikizi kutokana na umbali na changamoto za mvua kipindi cha masika, kukosekana Kwa huduma ya zahanati vijiji vya mbali ambapo wamesema kuondolewa kwa kero hizo kutarahisisha maisha yao na kuwakwamua kiuchumi pia.Hayo yamesemwa katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Thomas Apson leo tarehe 08 Mei, 2024 katika ziara yake Kijiji Cha Iglansoni ambapo kero hizo zimepatiwa ufumbuzi na kuwaagiza wakuu wa idara na vitengo alioongozana nao kuyachukua yanahitaji utekelezaji na kuyatatua kwa haraka.Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya amewaomba wanachi wa kijiji hicho pamoja na viunga vyake kushiriki kikamilifu katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwani mwenge huo upo kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan "Hivyo tujitikeze Kwa wingi ili kusema asante na kumuunga mkono Mama yetu mpendwa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan" ameongeza Mkuu wa Wilaya Aidha amesema Mwenge wa Uhuru utapokelewa Wilaya ya Ikungi tarehe 07 Julai, 2024, utakagua miradi na kukesha kijiji cha Pumba na baadae kukabidhiwa tarehe 08 Julai, 2024 katika Wilaya nyingine Kwa ajili ya kuendelea na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Singida.Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM katika kata ya Iglansoni Mhe.Emmanuel Bulugu pamoja na Diwani kata ya Iglansoni Mhe Yusuph Athumani wamesema kuwa viongozi wa Wilaya ya Ikungi inajitahidi kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapindizi na kuwaomba kuongeza juhudi katika utekelezaji wa ilani hiyo kwani ndicho kipimo kizuri kwa utendaji kazi wa watumishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa