Uwajibikaji kwa jamii (Corporate Social Responsibility - CSR) ni jukumu la kisheria na kijamii linalowahimiza wawekezaji na mashirika kuchangia maendeleo ya jamii kwa kupitia miradi mbalimbali kama elimu, afya, na miundombinu.
Katika muktadha huo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson, ameagiza kufanyika kwa kikao kati ya wawekezaji na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ili kujadili mikakati ya wawekezaji kuhusu utekelezaji wa CSR.
Akizungumza katika Baraza la Madiwani lililokuwa likijadili rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, Mhe. Apson alisema kuna umuhimu wa kufahamu mikakati ya wawekezaji ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na inaleta manufaa kwa jamii.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mhe. Ally J. Mwanga, alieleza kuwa kutoletwa kwa taarifa za CSR katika baraza la madiwani haileti picha nzuri, kwani baraza hilo ndilo lenye mamlaka ya kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya jamii.
"Uwajibikaji wa kijamii (CSR) sio hisani, bali ni takwa la kisheria. Wawekezaji wanapaswa kufahamu hilo na kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo," alisema Mhe. Mwanga
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa