Mkuu wa wilaya ya Ikungi kulia juu Mhe Thomas Apson amekabidhiwa rasmi wilaya hiyo na aliyekuwa Mkuu wa wilaya Ndg Jerry Muro tar 27 january 2023.
Katika makabidhiano hayo ndg Jerry Muro amesema anashukuru wana Ikungi kwa ushirikiano wao wakati wote wa kipindi cha utawala wake akiwa kama Mkuu wa wilaya,amesema tena kuwa ushirikiano huo huo wampe Mhe Thomas Apson ili Ikungi isonge mbele zaidi ya alipo achia yeye.
Pia katika makabidhiano hayo Mkuu wa wilaya amesema kuwa anamshukuru Mama Samia Suluhu Hassani kwa kumteuwa tena kuwa mkuu wa wilaya Ikungi mkoani Singida ,Amesema kuwa ataendeleza aliyoyaacha Ndg Muro na kuanza na mkakati wa ukatili wa kijinsia haswa kwa watoto na wanawake.
Katika makabidhiano hayo Ndg Muro alimkabidhi Mhe Thomas nyaraka zote zinazousiana na wilaya hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa