Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi amefanya uzinduzi wa Kliniki Tembezi maalum (MOBILE CLINIC) ambayo inafadhiliwa na kuendeshwa na Taasisi ya YANURUNI FOUNDATION
Ambayo lengo la Kliniki hii ni kumsaidia Mama mjamzito pamoja mtoto chini ya Miaka mitano huduma ya Afya yenye kuzingatia ubora na kujali utu.
Pia ni kuwafikia wananchi waishio vijiji/Vitongoji ambavyo umbali wa vituo vya afya kutoka makazi ya wananchi ni kubwa kiasi cha mwananchi kufuata huduma ya Afya hadi umbali wa kilometa 30 - 50.
Hadi sasa kwa mwezi Januari 2023 Mradi umeweza kuwafikia wananchi wa vijiji 3 ambavyo ni Kijiji cha Mnyange , Chungu na Nkunikana, na wananchi takribani 500 wamepatiwa huduma hii wakiwemo wanaume 123, wanawake 215 kati yao 36 ni Wajawazito na 71 ni watoto chini ya miaka mitano.
Wagonjwa hao wote wameweza kupata huduma mbalimbali kama vile huduma za RCH, huduma za chanjo, huduma za matibabu ya kidaktari, ushauri nasaha na upimaji wa VVU, Full blood picture, Vipimo vya Sukari, Typhoid na Malaria.
Mwisho Mradi unatarajia upunguaji wa changamoto za maradhi na vifo vya mama mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano visababishwavyo na ufinyu wa huduma za afya wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua.
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Tarehe: 15 Februari,2023.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa