Afisa Elimu Sekondari Ndg Ngwano John Ngwano ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari mpya mradi wa Mpango wa kuboresha ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) unaojengwa kata ya Issuna kijiji cha Nkhuhi.Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo leo Tarehe 12 October 2023 amesema kuwa mradi unategemewa kukamilika Tarehe 30 mwezi wa 10 mwaka huu ambapo wanafunzi 250 kidato cha 1 na cha 3 kutoka shule ya sekondari Issuna watahamia na kuanza kupata Elimu katika shule hiyo mpya"Pia nategemea kuanza na walimu zaidi ya 7 katika Shule hiyo mpya ambapo wataanza kufundisha hapo"alizungumza Afisa Elimu.Zaidi ya Milioni 544.2 zinatumika katika ujenzi huo wa Madara 8, Ofisi 2 Jengo la utawala,Maabara 3 (Kemia,Biolojia na Fizikia) Jengo la Tehama,Maktaba, Matundu ya vyoo 10,Kichomea taka na kisima cha aridhini.Ameongeza na kuagiza mafundi kuwa makini katika kazi zao ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza endapo hawatakuwa makini katika hatua za umaliziaji.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa