Bohari ya Dawa kanda ya kati Dodoma (MSD) wakabidhi majenereta mawili kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Ikungi pamoja na Kitanda cha upasuaji kimoja ambapo Jenereta moja litatumika katika kituo cha afya Sepuka.
Akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa Bohari ya Dawa Kanda ya Kati Ndg Mwanshehe Juma leo hii Tarehe 20 Novemba 2023 amesema vifaa hivyo vimegharimu takribani milioni 73.9 ambavyo ni pamoja na mashine ya kutoa joto kwa watoto mbili ,Utra sound moja ,mashine ya kutolea uchafu katika upasuaji tatu ambapo moja itatumika Sepuka na nyingine Hospitali ya Wilaya ya Ikungi.
Akizunguma mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Mganga Mkuu Wilaya ya Ikungi Dkt Dorisilla amesema hii ilikua changamoto kwa kipindi kirefu hivyo kuletwa kwa vifaa hivyo itasaidia sana kuepukana na changamoto za umeme hasa wanapopata wagonjwa wanaohitaji matibabu ya haraka.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Mhe Mtaturu ameshukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujitahidi kuleta vifaa tiba Wilaya ya Ikungi ili kuboresha huduma za afya Kuwaomba wananchi kufika katika Hospitali ya Wilaya ya Ikungi kupata matibabu
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa