Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson awataka wamiliki wa maduka ya Dawa kutoa ushirikiano kwa viongozi pale panapokua na uhitaji huo lengo ikiwa ni kuepusha migogoro itokanayo na kukosekana kwa ushirikiano.Akizungumza na wamiliki wa maduka ya Dawa Ikungi Tarehe 18 Julai 2023 katika ukumbi wa Halmashauri katika kikao cha Mhe Thomas Apson amesisitiza ushirikiano na mshikamano kati ya wamiliki wa maduka na viongozi wa serikali."Sisi na ninyi sio maadui tufanye kazi zetu kwa ushirikiano mfano swala la mapato na kutunzaji mzuri wa Dawa Ili kutoleta madhara kwa wananchi"Aidha amewataka wamiliki kuzingatia usafi na ubora wa bidhaa zao pamoja na umbali uliowekwa kisheria kati ya duka moja na lingine.Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha Msemo Afisa kilimo amesema kuwa uwepo wa chama cha wamiliki wa maduka ya Dawa kunawezesha kufanya kazi kwa ushirikiano.Kikao kiliratibiwa na Mfamasia wa Wilaya Mariam Mkomwa,Peter Mgana Mratibu wa huduma za MaabaraPamoja na viongozi mbalimbali kutoka Mkoani na Taifa.MWISHOAfisa HabariHalmashauri ya Wilaya18/07/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa