Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg.Kastory Msigala ameagiza kutungwa kwa sheria ndogondogo kudhibiti chumvi inayochimbwa kata ya Kikio pamoja na Misughaa kusambazwa bila kibali ili kuzingatia ubora wa chumvi kwa lishe bora.
Hayo yamesemwa hii leo tarehe 09 Mei, 2025 katika kikao cha kamati ya lishe kulichofanyika ukumbi wa Halmshauri hii ni kutokana na ukosefu wa madini joto katika chumvi inayozalishwa kata ya kikio na Misughaa ili isilete madhara kwa wananchi na kuzingatia ubora wa bidhaa hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji ameagiza kuwa jukumu la uchakataji wa sheria hizo pamoja na uratibu wa zoezi la uchimbaji wa chumvi kata ya kikio na Misughaa zitafanyika chini ya divisheni ya afya, viwanda na biashara, pamoja na divisheni ya sheria.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa kamati ya lishe wametoa maoni yao juu ya umuhimu wa lishe katika jamii na kuiomba kamati hiyo kushirikiana vyema kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuzingatia lishe bora shuleni pamoja na jamii kwa ujumla.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa