Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe.Steven Petro Mtyana akimuwakilisha mbunge wa jimbo la Singida mashariki amekabidhi vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya zaidi ya milioni 14 Kwa ajili ya kuinua taaluma shule ya Sekondari Ikungi na ufanisi kwa walimu.Akikabidhi vifaa hivyo leo katika mahafali ya 10 ya kidato cha sita shule ya sekondari Ikungi Makamu Mwenyekiti amesema kuwa vifaa hivyo ni pamoja na kompyuta tatu vitunza umeme vitatu pamoja na projecta moja ili kuwezesha katika ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule hiyo.Aidha ameongeza na kusema kuwa katika taarifa ya Mkuu wa shule ambayo imesomwa mbele yake imezungumza juu ya ufaulu wa hali ya juu Kwa miaka kadhaa iliyopita na kuomba wahitimu kuhakikisha historia hiyo nzuri haivunjiki ili kuongeza wasomi wengi zaidi nchini watakaosaidia taifa letu.Kwa upande wake Katibu wa Mbunge wa jimbo la Singida mashariki Mhe.Ally amesema kuwa hivi ni baadhi tu ya vifaa vya TEHAMA ambavyo Mhe. Mtaturu anatarajia kuvileta katika shule hii pamoja na shule zingine zilizopo katika jimbo lake kwani kumekuwa na changamoto kubwa katika baadhi ya shule ya uwepo wa vifaa wezeshi kwenye ujifunzaji."Tumeona hapa kwenye taarifa ya mkuu wa shule inasema bado kuna uhitaji mkubwa wa vifaa vingine kama printa na vingine hivyo nitalifikisha hilo Kwa ajili ya utekelezaji pia Mbunge ameahidi ndani ya muda mfupi ataleta runinga kubwa katika ukumbi wa shule hii Kwa ajili ya Burudani na kujifunzia na kutazama taarifa muhimu" amezungumza katibu wa mbunge
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa