Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson aipongeza serikali kwa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya amali Samamba ambayo inatarajiwa kugharimu zaidi ya Milioni 544, na kuwa msaada hasa kwa watoto wakike kuepusha matukio ya kikatili.
Hayo yamesemwa hii leo tarehe 01 Machi, 2025 katika zoezi la usafi wa mazingira na upandaji miti katika mazingira ya shule hiyo mpya kuelekea siku ya mwanamke duniani inayotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 8 mwezi huu.
Mhe. Apson amesema kuwa wanafunzi wa kata hiyo ya Kituntu wamekuwa wakienda umbali mrefu hiyo kusababisha mimba za utotoni na unyanyasaji wa kijinsi unaopelekea watoto hao kutomaliza masomo na kukatisha ndoto zao.
"Hivyo ujenzi wa shule hiyo inaenda kuwa suluhisho la matatizo ya namna hiyo" amesama Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii Bi.Haika Massawe akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Kastori Msigala amesema timu kutoka Halmshauri imekuwa ikifanya ziara katika maeneo kadha wa kadha kutoa msaada wa kisheria pamoja na kutoa elimu ya mkopo wa asilimia kumi za Mama Samia.
Amesema lengo la ziara hizo hasa kipindi hiki kuelekea siku ya wanawake duniani ni kutoa elimu kwa wananchi na wanafunzi pia ili wajue haki zao za msingi na sheria kwa ujumla.
Hata hivyo tumzungumza na baadhi ya wananchi wa eneo hilo wameishukuru serikali kwa ujenzi wa shule hiyo ya sekondari ya ufundi kwani inaenda kuamsha hari na ujuzi wa wanafunzi wenye vipaji mbalimbali vya ubunifu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa