Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Mhe.Rashid M.Rashid ahutubia wananchi wa Wilaya ya Ikungi akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson katika kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Mhe. Rashid amesema viongozi waasisi wa nchi ya Tanzania wameacha tunu katika taifa hili, hivyo ni wajibu wetu kudumisha, kuimarisha na kuuenzi muungano huu kwani tukiuelewa umuhimu wa muungano tutaulinda ili kukuza maendeleo nchini.Katibu Tawala ameongeza na kusema kuwa tarehe 22 mwezi aprili mwaka 1964 hati ya makubaliano ya muungano ilisainiwa rasmi na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Shekhe Aman Abeid Karume na kufuatiwa na matukio mbalimbali yaliyohitimishwa tarehe 26 Aprili 1964 Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kiwilaya ukumbi wa Halmashauri ya Ikungi hii leo tarehe 26 Aprili 2024, majadilioano mbalimbali juu ya dhana ya muungano yaliibuka huku badhi ya wajumbe kugusia juu ya umuhimu wa muungano huo unavyoleta matokeo chanya Kwa taifa letu Baadhi ya wajumbe wametaja umuhimu wa muungano huo ni pamoja na kuongezeka kwa ajira, kukuza umoja na mshikamano pamoja na kukua kwa maendeleo nchini Tanzania Mwalimu Adam shule ya sekondari akinukuu maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere amesema kuwa kinachotengeneza muungano sio sheria ila sheria imewekwa kwa lengo la Kulinda na kudhibiti muungano"Tumekuwa na mafanikio katika nyanja za ulinzi na usalama, pia muungano umezingatia usawa wa kijinsia nchini kwani kufanya hivyo kunafanya watu wote wawe sawa" amezungumza Mwalimu Adam.Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi katika shule ya sekondari Ikungi wamekuwa na mtazamo chanya juu ya serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuwaalika katika makongamano mbalimbali na matukio ya kiserikali kwani hiyo imekuwa ikiwajengea uwezo wa kuelewa mambo mengi yanayo wahusu wao na jamii kwa ujumla wake.Kauli mbinu ya maadhimisho hata ni miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania tumeshikamana, tumeimarika kwa maendeleo ya taifa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa