Mkazi wa kijiji cha Mtavira Bwana Sambali Ngelela ametoa ekari kumi na mbili kwaajili ya ujenzi wa shule ya msingi mpya Ituru.
Katika ziara ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Matha Mlata ya tarehe 6 julai 2023 wilaya ya Ikungi amempongeza mkazi huyo aliyeamua kutoa ardhi yenye ukubwa wa ekari 12 bure kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya Ituru ambapo ujenzi wake upo hatua za umaliziaji .
Mhe Matha Mlata ameagiza kutengenezwa kwa barabara inayoelekea shuleni hapo pamoja na umeme na maji lengo ikiwa ni kuwarahisishia wanafunzi kupata huduma kwa urahisi zaidi wakiwa shuleni.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson amewaomba wananchi kujitoa katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii hususani katika ujenzi wa madarasa wilayani hapa .
Kamati ya siasa mkoa wa Singida imefanya ziara hiyo katika shule ya sekondari Makilawa kuona ujenzi wa shule mpya ambayo imegharimu milioni 470 na imekamilika na imeanza kunatumika rasmi ,ujenzi wa josho lililo gharimu milioni 23 na shule ya msingi mpya ya Ituru iliyogharimu milioni 493.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa