Mwenge wa uhuru umetembelea mradi wa Kitalu cha miche tarehe 07 Julai, 2024 katika Wilaya ya Ikungi na kuridhishwa na mradi huo.
Akizungumz mara baada ya kukagua kitalu hicho cha uzalishaji wa miche ya aina mbalimbali katika shule ya msingi Ikungi Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg. Godfrey Eliakimu Mzava amesema kuwa kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka 2024 inahusu utunzaji wa mazingira hivyo Ikungi wanafata na kuitekeleza vyema kauli mbiu hiyo.Akisoma taarifa ya mradi huo Bwana Philbert Benedict Mradi maliasiri na uhifadhi wa mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi amesema kuwa mradi huu wa Kitalu cha Miche umeanzishwa mwezi Mei 2024 kwa lengo la kuzalisha miche kwa ajili ya kupanda katika maeneo ya shule hiyo na shule za jirani pamoja na maeneo mbalimbali ya wilaya ya Ikungi na unatekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Bwana Philbert amesema kuwa mradi unatarajiwa kutumia jumla ya Shilingi. 4,800,000 ambapo jumla ya miche ya miti 50,000 ya aina mbalimbali ikiwemo miti ya matunda, mbao na kivuli inatarajiwa kuzalishwa na hadi sasa, jumla ya Shilingi 4,150,000 imekwisha tumika na jumla ya miche 46,800 imeoteshwa na zoezi linaendelea.Ameeleza kuwa faida za mradi huu ni kuzalisha miche ya aina mbalimbali kwa ajili ya kupanda kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayotokana na uharibifu wa mazingira, kuzalisha miche ya kupanda kwa ajili ya matunda kwa lengo la kuboresha lishe na afya za wananchi, kuzalisha miche ya kupanda kwa ajili ya kutunza vyanzo vya maji, kurudisha uoto uliopotea kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu kama kilimo, ufugaji, na shughuli nyingine za maendeleo.MWISHO@samia_suluhu_hassan @gersonmsigwa @ikulu_mawasiliano @tbctaifa @singidars @singidamc
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa