Mwenge wa uhuru waridhishwa na mradi wa vijana wa ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali mara baada ya kutembelea mradi huo tarehe 07 Julai, 2024Kiongozi wa mwenge wa uhuru mwaka 2024 Ndg. Godfrey Eliakimu Mzava amesema kuwa ipo haja ya kuendeleza miradi mbalimbali ya vijana ili kukuza maendelo kwa kasi wilayani hapa
Akisoma taarifa ya mradi huo mwenyekiti wa kikundi cha Save The Bees kilishoanzishwa na kusajiliwa tarehe 29/5/2020 kwa namba IDC/CSO/1055 kikiwa na wanakikundi 11 wanaume 7 na wanawake 4. Kwa sasa kikundi kina wanakikundi 10 wanaume 7 na wanawake 3 na mlezi 1.Mwenekiti amesema kuwa Kikundi kinajishughulisha na ufugaji wa nyuki, uchakataji na uuzaji wa asali na kina shamba la ekari 30 katika Kijiji cha Issuna ‘A’ kitongoji cha Itintimo ikiwemo mizinga 60 ya kisasa na mizinga mingine 190 iko kwenye mashamba ya wanajamii. Mavuno ya asali hadi sasa ni wastani wa tani 1.
Ameongeza kwa kusema kuwa Mradi unagharama ya Shilingi 39,686,000 kwa mchanganuo Shilingi 3,000,000 ni mkopo kutoka 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri Shilingi 4,700,000 mchango wa Halmashauri kukarabati jengo, Shilingi 24,486,000 mchango wa Wahisani - shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO) Shilingi. 7,500,000 mchango wa wanakikundi.„Tumepata mafunzo ya mbinu bora za ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali toka Serikalini na wadau wengine na Kupitia kikundi, tumefaidika kwa wanachama kupata kujiajiri na kujiongezea kipato Kuhudumia wananchi kwa asali bora” amezungumza mwenyekiti huyo.@samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango @kassim_m_majaliwa @tbctaifa @itvtz
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa