Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ndg Bilinith Mahenge mnamo Octoba 27,2023 ametembelea wilaya ya Ikungi katika mgodi wa Shanta kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji wa ndani wenye masharti nafuu.Katika ziara hiyo amesema kuwa wazawa wanahamasishwa kuwekeza katika ardhi yao lengo kukuza Uchumi wetu na kujiajiri wenyewe kwa kutumia rasilimali zetu. Pia katika ziara hiyo uongozi wa Shanta wametupitisha katika maeneo mbalimbali ya mgodi huo na kutoa elimu kuhusu mgodi huo na namna unavyofanya kazi .Mwisho mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji ndg Richard Rwehumbiza ametoa ushirikiano mkubwa kwa ugeni huo kwa kuwapa taarifa fupi ya namna wanavyofaidika na mgodi huo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa