Mwenyekiti wa UWT Taifa Mhe Mary Chatandi aipongeza wilaya ya Ikungi na kusema kuwa ameridhishwa Ubora na ukamilishaji kwa wakati miradi ya maendeleo inayojengwa na serikali ikiwa ni moja ya utekelezaji ya Ilani ya chama cha mapinduzi.Hayo yamesema leo Tarehe 11 Agosti,2023 katika ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Ikungi Ikiwemo hospitali ya Wilaya ya Ikungi,Shule ya sekondari Mwau,Kituo cha Afya Mng'onyi na baadae alifanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Sambaru.Mwenyekiti UWT amesema kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatenga fedha nyingi za miradi hivyo hatuna budi kuzisimamia kwa ukaribu ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kutoa fursa ya kutengewa fedha zingine za miradi.Aidha Mganga mkuu wa wilaya ya Ikungi Dkt Dorisila Mlenga John wakati akisoma taarifa yake mbele ya Mwenyekiti ambaye ndiye alikua mgeni rasmi katika ziara hiyo amesema kuwa majengo yote yapo hatua za mwisho katika ujenzi na kufikia mwishoni mwa mwezi huu yote yatakua tayari na kuanza kutumika rasmi.Mganga mkuu ameongeza na kusema kuwa kuna upungufu wa watumishi katika hospitali hiyo ukilinganisha na idadi ya wagonjwa inavyoongezeka hivyo anaomba kuongezewa watumishi ili kukidhi mahitaji.Mwisho Mhe Miraji Mtaturu ameahidi kushirikiana vyema na uongozi wa wilaya na serikali kwa ujumla kuhakikisha miradi mbalimbali inatekelezwa hasa katika jimbo lake la Mashariki na kukuza maendeleo kwa wananchi.Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi11/08/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa