Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Deogratius J. Ndejembi na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -TAMISEMI anayesimamia Elimu, Dkt. Charles Msonde pamoja na timu yake wamefika hospitali ya Wilaya ya Ikungi Kukagua kasi ya utekelezaji Maelezo ya Katibu Mkuu w Chama cha Mapinduzi CCM aliyoyatoa wakati alipotembea hospitali hiyo tarehe 28 Februari 2023, hasa majengo yautoaju wa huduma hospitalini hapo...Awali Katibu mkuu alipongeza juhudi za Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kupokea baadhi ya vifaa vya hospitali na kuvifunga kwa ajili ya kuanza kutoa huduma na kusaidia kutatatua changamoto mbalimbali zilizo ndani ya uwezo wao na kutoa maagizo kuwa fedha za miradi zije ili kukamilisha ujenzi na baadhi ya vifaa ili hospitali hiyo iweze kuhudumia wagonjwa wengi na kwa uharaka... Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Ikungi Dr. Kahabi Madoshi Kimotoli akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi Ngd Daniel Chongolo alisema baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ni pamoja na Kutokamilika kwa majengo nane (8) Jengo la OPD, Maabara, Famasi, Utawala, Mionzi, Kufulia, Wodi ya wazazi na kichomea taka baada fedha kiasi cha Tshs 325,193,815/= zilizovuka mwaka wa fedha 2019/2020 kuchukuliwa na Wizara ya fedha na Mipango. Halmashauri imewasiliana na OR-TAMISEMI kuomba fedha za umaliziaji wa majengo hayo kama maelekezo yalivyotolewa na Mh.Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa ziara yake aliyoifanya WIlaya ya Ikungi tarehe 05/08/2022.Naibu waziri pamoja na katibu mkuu ofisi ya Rais wamekagua hospitali hiyo na kufanya tathini ya namna ya kutatua changamoto ambazo zipo katika hospitali hiyo...Aidha ugeni huo ulipata wasaa wa kuzungumza na baadhi ya wahudumu waliokwepo na kuwataka kufanya kazi kwa bidii bila kujali uhaba wa vifaa kwani serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan ipo tayari kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa wakati.Wenyeji wa ugeni huo walikua ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi, Mganga mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Michael Solomon pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Ikungi Dr. Kahabi Madoshi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa