Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson ameongea na wananchi wa Kata ya Issuna,Kusikiliza kero za wananchi na kutatua migogoro mbalimbali inayowakabili.Tarehe 3 Octoba ,2023 kabla ya kikao hicho Mkuu wa Wilaya ametembelea Shule mpya ya Sekondari ya Nkuhi na kupongeza kamati kwa utekelezaji wa ujenzi huo kwa asilimia mia moja.Baada ya ziara hiyo Mhe Apson amefanya kikao na wananchi wa kijiji cha Issuna B na kutatua migogoro yao ya maji ,vikao vya kijiji na matatizo ya kijamii kwa ujumla.Pia katika kikao hicho Mhe Apson amesisitiza wanachi kuchukua pembejeo za kilimo kama vile mbegu na mbolea ya ruzuku mapema kabla ya msimu wa kilimo kuanza na kuahidi pembejeo hizo kuwafikia mahali walipo wakulima hao.Mwisho Afisa kutoka RUWASA ametatua mgogoro wa maji kutokutoka katika kata ya Issuna ,na kusema kuwa miundo mbinu inatakiwa kufanyiwa marekekebisho muda wowote kuanzia sasa kwani wapo kwenye hatua ya ununuzi wa mabomba.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa