Na mwandishi wetu.
Mhe Dr Benelith Mahenge Mkuu wa Mkoa wa Singida Oct 19 amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Ikungi ambapo ametembelea Miradi ya Maendeleo ikiwemo Scheme ya Umwagiliaji Mang'onyi na kukagua Ujenzi wa Madarasa katika Sekondari ya Mwau.
Sambamba na hayo Amezindua rasmi Msimu wa Kilimo katika Mkoa wa Singida wakati akihutubia Wananchi wa kata ya Issuna.
Mhe RC amepongeza Ushirikiano uliopo baina ya Viongozi ngazi ya Wilaya wakiongozwa na Mhe DC Jerry Muro na Mkurugenzi Mhe Justice Kijazi huku akisisitiza mshikamano uliopo uendelee kudumu kwa maslahi ya Maendeleo ya Wananchi wa Wilaya ya Ikungi na Taifa kwa Ujumla.
Picha za matukio
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa