MKUU wa mkoa singida Mhe Peter Serukamba amewapa maelekezo wakuu wa wilaya wapya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kukuza mapato katika wilaya zao ili kuleta maendeleo endelevu mkoa wa Singida.
Akizungumza katika hotuba yake hii leo tarehe 07 februari 2023 wakuu wa wilaya wanne walioteuliwa kuja Mkoa wa Singida amewaagiza kukuza ukusanyaji mapato na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Singida kubwa zaidi ikiwa ni pamoja na migogoro ya ardhi, kukuza maendeleo kwa mwananchi pamoja na miundo mbinu...
Ameongeza na kusema kuwa namna pekee ya kutatua changamoto hizo ni kuimarisha mshikamano na ushirikiano baina ya watumishi na wananchi na kudhibiti vitendo vya rushwa ili kutoa haki kwa Kila anayestahili
Aidha amewata wakuu hao wa wilaya kusimamia kilimo na upandaji wa miti ili wakulima waendelee kuongeza maeneo ya kulima huku akibainisha kwamba Mkoa wa Singida umekua Mkoa wa pili kwa kuongeza eneo la kilimo ukiondoa Mkoa wa Morogoro.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa