Mkuu wa Mkoa Mhe Peter Serukamba aipongeza Wilaya Ikungi kwa hatua nzuri ya miradi inayojengwa na Serikali na kuwaagiza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi pamoja na Mkuu wa Wilaya Mhe Thomas Apson kusimamia kwa karibu miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati ifikapo tarehe 20 mwezi huu.Akizungumza katika ziara hiyo ya siku ya kwanza leo Tarehe 05 Juni 2023 kutembelea miradi mitano ikiwa ni pamoja na Kituo Cha afya Iglansoni kinachogharimu Zaidi ya milioni 500,mradi wa maji RUWASA Iglansoni unaogharimu milioni 287.1,Ujenzi wa Madarasa 2 na matundu matatu ya vyoo Shule ya Msingi Ilolo unaogharimu milioni 51.1,Ujenzi wa Daraja la Nduru ,Mradi wa maji Ihanja unaogharimu milioni 423.6 pamoja na bweni la wanafunzi sekondari ya Puma inalogharimu zaidi ya milioni 122.1 Mkuu wa mkoa amesema kuwa Serikali imetoa fedha nyingi kwa kipindi kifupi hivyo tunapaswa kuhakikisha fedha hizo zinatumika vizuri kukamilisha miradi hiyo.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika taarifa yake ameishukuru serikali kwa kuleta miradi mbalimbali katika Wilaya ya Ikungi na kuahidi kusimamia miradi hiyo iweze kukamikika kwa wakati kama maagizo ya mkuu wa mkoa katika ziara yake.Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson amewaomba viongozi wakata na vijiji kuhamasisha wananchi kushiriki katika ujenzi wa miradi kama usogezaji wa mchanga,maji,kokoto,matofali pamoja na kusafisha eneo la ujenzi hasa katika miradi ya shule mpya zinazojengwa wilaya ya Ikungi.Ziara hiyo ya siku mbili itaendelea kesho katika wilaya ya Ikungi ambapo Mkuu wa mkoa atatembelea miradi mingine kujiridhisha na kusisitiza ukamilishaji wa miradi hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa