Mkuu wa Divisheni ya Mazingira Halmashari ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Richard Rwehumbiza awasilisha utafiti wa pori la hifadhi Minyughe linalotarajiwa kutumika katika mradi wa hewa ya ukaa pale taratibu zitakapokamilika.
Utafiti huo umefafanua ukubwa wa eneo, aina ya miti inayopatikana katika msitu huo, shughuli za binadamu zinazoathiri hifadhi, na kiasi cha hewa ya ukaa kinachopatikana kupitia msitu huo, ujazo, maumbile, mabadiliko ya msitu na uhifadhi wa msitu.
Akifafanua utafiti huo kiongozi kutoka NEMC amesema kuwa ripoti imetaja aina ya miti iliyopo katika msituhuo kuwa ni pamoja na Miombo, vichaka na miti mingine inayozalisha hewa ya ukaa zaidi ya tani 23 kwa hekta na katika kila hekta ya miombo uwezo wa kuzalisha tani 28, hivyo kwa utafiti huo kuna uwezekano wa kuvuna tani nyingi kupitia msitu huo uliopo wilaya ya Ikungi.
“Zaidi ya asilimia 75 msitu unafaa kwa uzapishaji wa hewa ya hewa ya ukaa pamoja na shughuli zingine zisizoathiri uaribifu wa misitu kama udugaji wa nyuki wa asali” amezungumza Mtafiti kutoka NEMC
Utafiti huo umefanywa na kamati maalumu yenye wajumbe kutoka NEMC, Halmashauari, TFS pamoja na viongozi wa Mkoa na wametoa ushauri kuwa kuna haja ya kuanzishwa kwa sheria ndogo ndogo zinazodhibiti wavamizi wa misitu hiyo
Lengo la utafiti hii ni kuelekea kwenye biashara ya hewa ya ukaa ambapo baadhi ya makapuni yameonyesha nia ya kuwa na uhitiji wa kufanya biashara na Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa