Katika mkutano wa Tarehe 16 Octoba 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka vijana kuendeleza sekta ya nyuki kwani Ufugaji wa nyuki ni asili ya Watu wa Singida.Rais Samia amesema hilo baada ya kupata historia ya Singida wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Mkoa wa Singida kuwa ufugaji wa nyuki umeanza tangu enzi za mababu hivyo hatuna budi kuiendeleza asili hiyo.Aidha amemuagiza waziri mwenye dhamana ya sekta ya nyuki nchini kushirikiana na vijana wa singida kuikuza sekta hiyo ili kuleta maendeleo mkoani Singida.Kwa upande wake Ndg Philbert U.Benedict Afisa Nyuki Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi amesema kitengo cha nyuki kikishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi kinatekeleza mradi wa Kusaidia kuongeza Mnyororo wa thamani wa ufugaji wa Nyuki BEVAC ambao unawafikia wafugaji binafsi na wenye vikundi chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya."Tunatoa mafunzo kwa wafugaji zaidi ya 100 kuhusu mbinu za ufugaji kibiashara na ujasiriamali kupitia mazao ya nyuki"amesema PhilbertPia maeongeza na kusema kuwa Ikungi ina mradi wa kusaidia jamii zinazoishi pembezoni mwa misitu katika vijiji 10 ambavyo ni Ng'ongosoro,Iglanson,Minyughe,Mhintiri,Makilawa,Mtavira,Mpugizi,Mtunduru,Germani pamoja na Mwaru kujishughulisha na ufugaji wa Nyuki ili kupunguza kasi ya uharibifu wa misitu."Mradi huu unafadhiliwa na Mfuko wa uhifadhi wa misitu Tanzania FAFF"Amezungumza Afisa Nyuki Ndg PhilbertMwisho amesema kila mwaka kitengo hiki kinaweka kwenye bajeti shughuli za ufugaji wa nyuki lengo ikiwa ni kuboresha na kukuza sekta ya ufugaji wa nyuki Wilayani Ikungi.Imetolewa na:Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi23/10/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa