SENSA YA WATU NA MAKAZI -WILAYA IKUNGI YAFIKISHA ZAIDI YA ASILIMIA 85
Mkuu wa mkoa wa singida Mhe. Peter Serukamba ameridhishwa na jinsi wilaya ya Ikungi inayoendesha zoezi la sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022 leo jumamosi tarehe 27/08/2022, na kuitaka wilaya wamalize zoezi lote la sensa ya watu na makazi
Rc Serukamba amesema kama mpaka sasa wilaya imeshafikisha zaidi ya asilimia 85 kwa kuandikisha kaya zaidi ya elfu 51 kuna uwezokano mkubwa wakamaliza zoezi hilo mapema iwezekanavyo .
Ziara hio ya kutembelea wilaya ya Ikungi imetokana na kikao alichokifanya na wajumbe wa sense mkoa katika ofisi ya mkuu awa mkaoa tarehe 25/08/2022, ambapo alimwagiza mratibu wa sensa wa mkoa wa Singida ndugu Naing’oya kipuyo kuangalia na kuongeza Timu ya makarani ndani ya wilaya zao kuhakikisha zoezi hilo linaisha haraka na kwa wakati.
Wakati huo huo Rc Serukamba amewataka wasimamizi na waratibu wa sensa Ikungi kuwahamisha makarani waliomaliza katika maeneo yao na kuwapeleka kwenda kuongeza nguvu katika maeneo ambayo hayajafikiwa na yana idadi kubwa ya kaya uku zingine zikiwa kwenye umbali kufikiwa
Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi Ndugu Justice Kijazi amemuhakikishia Rc Serukamba kuwa zoezi litakwenda vizuri na litamalizika katika muda uliopangwa na kwa uadilifu mkubwa
Tazama picha za matukio
Pich aya pamoja mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. JERRY MURO (mwenye miwani) akizumgumza na afisa mipango wa Hlmashauri ya wilaya ya ikungi pamoja na msimamizi wa maudhui bi. Rachel Maliwa
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilwya ya Ikungi ndugu . Justice Kijazi akisoma taarifa ya sense ya watu na makazi inayoendelea wilaya ya Ikungi
Mkuu wa wmkoa wa Singida Mheshimiwa Peter Serukamba akiwa anaweka msisitizo unaohusiana na mwendelezo wa Sensa mkoa wa Singida na wilaya ya Ikungi
mkuu wa mkoa wa singida Ndugu Peter Serukamba akiweka masisitizo wa Zoezi la sensa ya watu na makazi
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Murro akiwa pamoja na Afisa mipango wa Hlmashauri ya wilaya ya Ikungi na Msimamizi wa maudhui wakijadili jambo
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya IKUNGI Ndugu Justice Kijazi akisoma taarifa za sensa
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa