Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe Peter Serukamba amewataka viongozi wa kijiji cha choda kata ya choda wilaya ya Ikungi kumpa ushirikiano Mwenyekiti wa kijiji hicho na kuepukana na maslahi binafsi ambayo yanasababisha migogoro katika kijiji hicho...
Akizungumza na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya kijiji hicho tarehe 02 Novemba , 2022 Serukamba alisema kuwa viongozi wanapaswa kujua majukumu yao, kuwa na mahusiano mazuri na wananchi wao lakini pia wanapaswa kusoma mapato na matumizi ya fedha za umma lengo ikiwa ni kuepusha migogoro itokanayo na maswala ya fedha."kwa maelezo niliyoyapata hayana uzito wa kumuondoa mwenyekiti Ndg Charles
Elias madarakani waiteni wananchi mmalize migogoro yenu". alisema Serukamba.
Aidha mkuu wa mkoa amewapongeza Mkuu wa wilaya Ndg Jerry Murro pamoja na MKurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ikungi Ndg Justice Kijazi kwa juhudi zao kutaka kumaliza mgogoro huo uliojitokeza tangu awali.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa