Shamba darasa la vijana lililotengenezwa katika Ofisi ya Halmashauri ya Ikungi lashamiri na kutoa mazao lukuki. Pichani kushoto ni Mkuu wa Mkoa Dkt. Bilinith Mahenge, wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya Mhe. Jerry Muro katikati ni Mwenyekiti wa kikundi cha vijana. Mkuu wa Mkoa ametoa agizo kwa Halmashauri zote Mkoani Singida kuhakikisha wanatekeleza agizo la Waziri Mkuu la kulima mazao ya mfano kwenye vitalu nyumba ili kuwafundisha vijana kujiajiri wenyewe kwenye kilimo kwa kutumia njia mbadala ya kilimo cha umwagiliaji wa matone . Ikungi imekuwa mfano wa kilimo hicho kijulikanacho kwa jina la "green house"
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa