Kampuni ya Shanta Mine inayojishughulisha na shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini wilayani Ikungi, Wametoa Msaada wa barakoa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Jana tarehe 24/04/2020.
Katika hafla ya ugawaji wa msaada huo , kwa niaba ya kampuni ya Shanta Mine, mwakilishi alisema
" tunatoa msaada huu wa barakoa hizi kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa maambukizi ya virusi vya korona. Pia tupo mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za Mh Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID19"
Hafla hiyo ilifanyika katika jengo la Halmashauri ya wilaya ya Ikungi na kuhudhuriwa na wakuu wa idara pamoja na watumishi wa makao makuu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa