Kamati ya Ulinzi wa wanawake na watoto MTAKUWA Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida waadhimia kutoa elimu juu ya janga la ukeketaji kupitia mikutano ya kata na vijiji Pamoja na kutumia viongozi wa dini lengo ikiwa ni kutokomeza ukeketaji asilimia 30 uliopo katika Mkoa huo...
Maadhimio hayo yamefanyika hii leo tarehe 12 Octoba katika kikao cha kamati hiyo kilichofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali Empower Society Transform Lives (ESTL) lenye makao makuu yake Mkoa wa Singida walipokuwa wakifanya uzinduzi wake wilaya ya Ikungi lengo ikiwa ni kutokomeza janga la ukeketaji kupitia semina mbalimbali katika kata na Vijiji wilayani hapo...
Joshua Lissu ni Mkurugenzi wa ESTL Alisema kuwa mpango wa shirika hilo ni kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na watoto wakike."shirika hili limefanikiwa kutokomeza janga hili kwenye kata 28 katika Mkoa wa Singida kwa muda wa miaka minne tu" Alisema Mkurugenzi wa shirika hilo...
Aidha Mkurugenzi aliongeza na kusema kuwa shirika hilo limefanikiwa kuanzisha mfumo wa Tehama unaosaidia kufatilia kesi zinazohusu maswala ya unyanyasaji wa kijinsia...
Kwa Upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ikungi Bi Suzan Kidiku, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Richard Rwehumbiza Pamoja na kamati ya MKAKUWA wameahidi kushirikiana na Shirika hilo lisilo la kiserikali kupinga ukatili wa Wanawake na watoto wakike
Shirika la ESTL limeanzishwa mwaka 2011 na limeanza kutekeleza mipango mkakati yake mwaka 2018 mpaka sasa.
Afisa Habari
Halmashauri ya Ikungi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa