Afisa elimu msingi Bi Margaret Kapolesya amewataka walimu wakuu,maafisa elimu kata na wenyeviti wa bodi za shule kutoa elimu kwa wazazi wanayopata kupitia mafunzo ambayo yanalenga kuhamasisha elimu ya shule bora UWAWA.Akizungumza na walimu wakuu pamoja ana wenyeviti wa bodi za shule wa wilaya aya Ikungi tarehe 27 Februari 2023 kapolesya amesema pia katika kukuza elimu ni vyema kuwazingatia watoto wenye ulemavu pia mana wana haki za msingi katika kupata elimu.kwa upande wao baadhi ya watoa elimu wa mafunzo hayo ya UWAWA Ushirikiano wa walimu na wazazi Afisa maendeleo maenedeleo ya jamii Bi Haika Massawe amesema kuwa lengo la program ya shule bora ni kuinua ufaulu,kuboresha mazingira ya kujifunza ujumuishi katika utoaji wa elimu.Kwa upande wao walimu,wenyeviti wa bodi na maafisa elimu kata wamesema wanayafurahia mafunzo kwani yatasaidia kuwajenga wanafunzi pamoja na wazazi ili kukuza elimu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa