Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Bi-Wonfrida Funto awaomba wazazi na jamii kuwapenda,kuwathani,na kuwaendeleza watoto kwani ni wajibu wao...
Hayo yamesemwa leo Tarehe 11 Octoba 2022, alipokuwa akizungumza na watoto wakike katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyofanyika kiwilaya kata ya Ikungi na kusema kuwa siku ya mtoto wa kike inatoa fursa na kuongeza ufahamu juu ya ukosefu wa usawa wa kijinsia unaowakabili waschana kote ulimwenguni kulingana na jinsia zao."siku pia inaonyesha mafanikio mbalimbali kama uundaji wa sera upangaji programu na kampeni kusisitiza usawa wa kijinsia"Alisema Bi-Winfrida.
DAS huyo aliongeza na kusema kuwa wazazi na walezi hawana budi kuangalia upya mtazamo wao juu ya Hatima ya watoto wakike na kimarisha haki za watoto ili taifa kuwa na ustawi bora na kuongezeka kwa fursa za maendeleo Duniani...
Aidha aliwapongeza viongozi wa kata akiwemo Diwani wa tarafa ya Ikungi Bi-Magreth Philemon Chima pamoja,Balozi Bi-Nyasugara P. Kadege na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi Pamoja na Idara ya maendeleo ya jamii kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya ya kuandaa maadhimisho hayo...
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Wakati wetu ni sasa,Haki zetu,Hatima Yetu" na maadhimisho haya hufanyika kila mwaka Tarehe 11 Octoba.
Afisa Habari,
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa