Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson Ashiriki zoezi la Usafi wa Mazingira uliofanyika kiwilaya katika kijiji cha Puma na kuwataka wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya usafi kila siku na sio kusubiri siku maalumu zilizotengwa na serikali.Mhe Apson ameyasema hayo mapema hii leo katika siku ya Usafi duniani katika kijiji cha Puma mara baada ya usafi na kusisitiza usafi usifanyike kwenye mazingira pekee bali na miili yetu pia ili kuwa nadhifu muda wote.Kwa upande wake Afisa Mazingira Halmashuri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Richard Rwehumbiza akisoma taarifa mbele ya Mhe DC amesema Kiasi cha taka kinachozalishwa katika Halmashauri ya wilaya ya ikungi ni Tani 82,911.36 kwa mwaka na Wananchi wanashiriki kufanya usafi katika maeneo yao na maeneo ya wazi kila jumatano ya kila wiki na jumamosi ya mwisho ya kila mwezi kama agizo la serikali linavyosema.Afisa mazingira ameongeza na kusema kuwa Kiasi cha taka kinachokusanywa tani 41,455.68 sawa na asilimia 50% ni taka ambazo utupwa mashambani kama mbolea kwa kuwa zinatokana na mazao ya mashambani na kiasi cha taka tani 16,582.27sawa na asilimia 20% kinafukiwa na kiasi cha taka tani 16,582.27sawa na asilimia 20% kinatupwa Dampo na kwenye mashimo ambayo yameainishwa kama madampo na kiasi cha taka tani 8,291.14 sawa na asilimia 10% zinabaki mitaani kila mwaka. "Kwa mji wa ikungi tuna dampo ambalo lipo KM 4 kutoka katikati ya mji na lina urefu wa Mita 150 na upana wa Mita 63 ambalo linatumika kutupia taka kwa mji wa ikungi na Tume waagiza watendaji wa kata zote kutenga maeneo kwa ajili ya Dampo."amezungumza Afisa MazingiraMwisho Mhe Apson amepongeza juhudi za Mkurugenzi na Timu yake yote kuhakikisha vifaa vya kufanyia usafi vinapatikana muda wote na vinafanyiwa kazi.Siku ya usafishaji Duniani huadhimishwa Duniani kote tarehe 16 septemba kila mwaka na Siku hii iliadhimishwa kwa mara ya kwanza Duniani mwaka 2019 na nchini Tanzania mwaka 2022 Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (UN-HABITAT) kupitia kikao chake cha tarehe 5-9 Juni, 2023 kilichofanyika Jijini Nairobi, Kenya kilipitisha azimio namba HSP/HA.2/L6 la utekelezaji wa siku hii kwa nchi zote Wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa