Kamati ya ulinzi na usalama imewataka waganga wote wa jadi kujisajili ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuepukana na migogoro inayotokana na imani potofu.Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson tarehe 01 Juni 2023 katika kikao cha ndani na mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mnane katika Kata ya Kikio ambapo aliwataka wananchi kutojihusisha na Waganga wanaowachonganisha kwani inawashusha kiuchumi.Hii ni kutokana na malalamiko ambayo baadhi ya wananchi wa kikio wanasema kuna waganga wa kienyeji wanaofanya ramli chonganishi maarufu kama Lambalamba ambayo inapelekea kuleta migogoro kwa watu kuhusishwa na mambo ya kushirikina.Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mnane wamesema kuwa swala la lambalamba halikubaliki na linashusha uchumi wa wananchi wa Kikio "Hili ni tatizo la uelewa mdogo wa baadhi ya wananchi kutokuelewa madhara yatokanayo na ramli chonganishi"amesema Nobert Albet mwananchi.Nao viongozi wa dini wamewataka wananchi kumrudia Mwenyezi Mungu ili kuepukana na tatizo hili la ramli chonganishi.Vijiji vilivyoathiriwa na tatizo hili la lamba lamba ni pamoja na Kikio,Mnane,Simbikwa na Mphoghoo na wanafanya kazi katika misitu ya Mkungu wa kihendo.DC Thomas Apson pia ametembelea kijiji cha Muhintiri kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na baadhi kuzitatua ili kukuza maendeleo katika kijiji hicho.MWISHO Afisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi01/06/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa