Kamati ya fedha Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imepitia na kujadili tarifa ya hesabu za mwisho wa mwaka unaoishia Juni 30,2022...
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 27 septemba,2022 katika ukumbi wa halmasauri wilayani hapo kikiongozwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Bwana Ally J. Mwanga ...
Mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kuthibitisha ajenda za kikao maalumu cha kamati ya fedha,uongozi na mipango cha tarehe 27 septemba,2022.
Aidha kamati hiyo ilipitia na kujadili taarifa ya hesabu za mwisho wa mwaka unaoisha juni 30,2022.
kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ikungi Bi Haika Massawe na makamu mwenyekiti Mtyana S. Petro.
(Pichani ni Mwenyekiti,Makamu mwenyekiti, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi pamoja na wajumbe wa kamati ya fedha wakiwa kwenye kikao)
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa