Marehemu Mgonto, Diwani wa kata ya Siuyu alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu lililopelekea kifo chake.
Mnamo tarehe 26.11.2017 na kuzikwa kitongo cha NALI . Ameacha mjane, watoto 6, wajukuu 4.
MAISHA YA SIASA
Mh Mgonto, alikuwa mwanachama mwaminifu wa Chama Cha Mapinduzi katika muda wote wa uhai wake.
Mnamo tarehe 26/11/2017 aliibuka mshindi wa uchaguzi wa marudio wa udiwani kata ya Siuyu.
Mh. mgonto atakumbukwa na jamii kwa mchango wake mkubwa katika shughuli za kijamii , michezo na maendeleo kiujumla katika kata ya Siuyu na wilaya ya Ikungi kwa ujumla. mchango wa maendeleo ni kama kupeleka tofali na saruji katika shule ya siuyu, kutoa na kugawa mipira yenye thamani ya zaizi ya milioni moja na laki tano, pamoja n akuongoza ligi ya vijana.
pia itakumbukwa aliwezesha upatikanaji wa mradi mkubwa wa maji kijiji cha Unyagumpi, mradi wa umeme wa sola na maji kijiji cha Makotea, umalizaji wa darasa sekondari ya Siuyu yenye thamani ya shilingi milioni kumi na saba.
Bwana alitoa na bwana alitwaa . jina lake lihimidiwe.
PICHA NA MATUKIO YA PICHA
wakazi wa kata ya Siuyu waliohudhuria Msiba
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa